Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 29Article 560377

Habari Kuu of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: eatv.tv

Waziri ayaonya mashirika yasiyo ya kiserikali nchini

Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya

Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima, ameagiza mashirika yasiyo ya kiserikali kufanya kazi zilizoainishwa kwenye mikataba yao ya vibali na sio kukiuka misingi iliyowekwa na serikali.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo mapema leo Septemba 29, 2021, Jijini Dodoma kwenye mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo amebainishha kuwa baadhi ya mashirika hayatekelezi vizuri maazimio wanayokubaliana hivyo kukiuka taratibu zilizowekwa.

Katika hatua nyingine Dkt. Gwajima, amezindua mwongozo wa kisera wa mgawanyo wa majukumu yenye kipengele cha kuzuia ukatili wa kijinsia ambapo ameagiza vyombo vinavyolinda na kusimamia haki za binadamu nchini vijitahidi kusaidia makundi yanayokumbwa na manyanyaso mbalimbali.