Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 18Article 552235

Habari Kuu of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri wa Afya kazungumza kuhusu kauli ya IGP Sirro kutaka barua

Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima na Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima na Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima

Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto, Dorothy Gwajima, ametolea ufafanuzi kauli ya Mku wa Jeshi la polisi, IGP Simon Sirro, iliyokuwa ikimtaka Waziri huyo kufika kituo cha Polisi kwa ajili ya kufungua kesi yake dhidi ya mbunge wa jimbo la kawe, Josephat Gwajima anaedaiwa kutoa kauli zinazopinga juhudi za serikali za kuhamasiha wananchi kuchoma chanjo ya Corona.

Alifafanua kauli ya IGP, huku akiwataka watu waache kupotosha umma, kwa minong'ono ambayo haina mantiki kwani kiongozi huyo wa Jeshi la Polisi hajakaidi agizo lake bali ametaka taratibu zifuatwe.

"IGP yupo sawa kabisa, baada ya mimi kutamka hivyo,akasema sawa amesikia, lakini ni kwenye mitandao na kama ilivyo kawaida lazima tupeleke maandishi, sasa atawezaje kufanyia kazi jambo ambalo halipo kwenye maadishi? kwahiyo watu wasijifiche tu pale kwamba Waziri amekataliwa na IGP, ila IGP amesema karibu, taratibu zifuatwe, na tayari taratibu zimeshafanyika".

Waziri huyo alitoa agizo hilo hapo jana kwa vyombo vya dola likiwemo Jeshi la Polisi na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU, kuhakikisha wanamkamata mara moja mbunge huyo kwani amechoka kuvurugiwa Wizara kwa matamshi ya kupotosha yanayotolewa kila kukicha.