Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 07Article 584014

Habari Kuu of Friday, 7 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Waziri wa Fedha ateuwa wajumbe 12 Bodi ya Uhasibu

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Taifa Uhasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania.

Hatua hiyo ni baada ya Rais Samia Suluhu Hassan siku chache zilizopita kumteuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania, Sylvia Shayo Temu.

Aidha, Dk Mwigulu amewateuwa wafuatao kuwa wajumbe wa bodi hiyo. Profesa Ganka D Nyamsogoro, Issa Masoud Iddi, Aisha R Kipande, Paul R Bilabaye, Dyoya G.J.Dyoya.

Wengine ni Rukia H Abdullu, Rukia Adam, Witness Shelekirwa, Francis Mwakapalilwa, Frendrick B Msumari na John Florian Ndetico.