Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552652

Habari Kuu of Friday, 20 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri wa Fedha awataka watanzania kuvumilia tozo

Tozo za Miamala ya simu Tozo za Miamala ya simu

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amewataka Watanzania kuvumilia makato ya tozo za miamala ya simu, kwani bado wanaendelea kujadiliana ili kuweka mambo sawa kuhusu tozo hiyo.

Ametoa kauli hii mapema hii leo alipokuwa akizungumza kuhusu muafaka wa Tozo za Miamala ya simu, na kuongenzea kuwa kuwa anatarajia kukutana na watoa huduma wa mitandao ili kuweka mambo sawa kwa awatanzania wote.

“Waziri Mkuu atapanga na yeye kikao chake cha kusikiliza kisha tutakuwa na jambo la kuwaambia Watanzania, kwakuwa Watanzania wameendelea kuvumilia siku hizi zote na kuunga mkono Serikali tunaomba waendelee kuvumilia makato haya ya tozo kwa siku hizi chache"

“Leo nikitoka hapa nitakuwa na kikao kuendelea kuweka hizi namba sawa, sio muda mrefu tutatoa tamko ambalo linahusiana na frame work ambayo ina hatua nzuri zaidi, linalohusisha namba ambazo zimeangaliwa kati yetu sisi na wenzetu (watoa huduma za mitandao) ili kuweka mambo sawa“