Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 17Article 551920

Habari Kuu of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri wa zamani, Basil Mramba Afariki dunia

Waziri wa Fedha wa zamani, Basil Pesambili Mramba Waziri wa Fedha wa zamani, Basil Pesambili Mramba

Aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha wa Tanzania, Basil Pesambili Mramba amefariki dunia leo Jumanne, Agosti 17, 2021 katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu.

Mramba aliwahi kuwa Waziri wa Fedha katika utawala wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambapo aliiongoza Wizara hiyo mwaka 2001-2005, baadaye Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko mwaka 2006 hadi 2008.

Kwa mujibu wa familia ya Mramba imeelezwa kuwa Waziri huyo wa zamani amefariki kwa Corona hivyo na kuhitaji wanafamilia wachache tu watakaoruhusiwa kufika kutoa pole nyumbani kwa marehemu, Mawenzi Road, Oysterbay Dar es Salaam