Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 13Article 551314

Habari Kuu of Friday, 13 August 2021

Chanzo: AP

Wenye “Kinga Hafifu” ruksa kuchoma chanjo ya nyongeza

Wenye “Kinga Hafifu” ruksa kuchoma chanjo ya nyongeza Wenye “Kinga Hafifu” ruksa kuchoma chanjo ya nyongeza

Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Marekani (FDA) imetoa idhini kwa watu wenye kinga hafifu kutafuta chanjo ya nyongeza ili kujilinda zaidi na kirusi cha COVID-19 hasa Delta.

Taarifa hiyo iliyotolewa Alhamisi August 12, 2021 imesema kutokana na kuwepo kwa watu wenye upungufu wa kinga kwenye miili ya kulikosababisha na matumizi makubwa ya madawa makali, wagonjwa wa Kansa, waliofanyiwa upasuaji wa kupandikiza viungo na wenye hitilafu zozote kali za kiafya, wanaruhusiwa kuongeza chanjo ya ziada ili kujilinda zaidi na kirusi cha Delta.

Nchi nyingine zilizoagiza wananchi wake kuongeza chanjo ya ziada ni pamoja na Ufaransa na Israel.

Imeelezwa kuwa ni ngumu kufufua mfumo wa Kinga uliathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na matumizi ya madawa makali au magonjwa hivyo pamoja na kuchanja bado kundi hilo linakua kwenye hatari ya kuathirika na COVID-19 ukilinganisha na wale wenye kinga imara. “Kwa maelezo hayo sasa ni bora watu wenye kinga hafifu waongeze chanjo ya ziada”. Amesema Dr. Rochelle Walensky Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magongwa CDCP.

CDCP imeaongeza kuwa chanjo ya nyongeza itawahusu wale wenye matatizo ya kiafya na kinga hafifu pekee na sio kwa watu wote wanaotaka kuongeza kinga. Kwa mujibu wa takwimu Marekani ina 3% ya watu wenye matatizo ya kiafya yanayohitaji kupata kinga ya ziada.

Nchini Ufaransa tayari Mamlaka zilishaanza kutelekeza uchanjaji wa kinga ya ziada ya tatu au ya pili kwa wananchi wake kuanzia mwezi Aprili mwaka huu.