Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 26Article 553912

Habari za Afya of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Wilaya hizi 11 zimetakiwa kutoa maelezo kwa kuhusu tatizo la "Lishe Duni"

Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu, amezitaka Halmashauri 11 nchini kutoa maelezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI ndani siku 14, ni kwa nini wametekeleza mpango wa Lishe kwa kiwango cha asilimia 25.

Waziri Ummy, ametoa maaagizo hayo, leo Agosti, 26, 2021, wakati akifungua Mkutano wa Tano wa Kupitia Afua za Lishe, unaofanyika mkoani Shinyanga katika Manipaa ya Kahama, ambapo amesema lengo la Serikali nikuona nchi inaondokana na suala la uatapiamlo na udumavu wananchi wake.

“Nizitake Halmashauri za Wilaya ya Tarime, Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Halmashauri Wilaya Buhigwe mkoani Kigoma, Halmashauri ya Handeni Mji mkoani Tanga, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita, Halmashauri ya Manispaa Shinyanga mkoani Shinyanga, Halmashauri Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora mkoani Tabora, Halmashauri Wilaya ya Ileje mkoani Mbeya na Halmashauri Wilaya ya Itigi mkoani Singida zitoe maelezo kwa katibu Mkuu TAMISEMI ndani ya Siku 14” Alizitaja Waziri Ummy.

Mbali na maelekezo hayo, hakusita kuwapongeza Wakuu wa Mikoa kwa kuhakikisha ongezeko la utoaji ya fedha kwa ajili ya kutekeleza mpango huo, kutoka asilimia 22 kwa mwaka wa fedha 2017/18, asilimia 52 kwa mwaka wa fedha 2019/20 na kufikia asilimia 57 kwa mwaka wa fedha 2020/21.