Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 19Article 552403

Uhalifu & Adhabu of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Wizi vifaa vya reli wawafikisha mbaroni wanne

Wizi vifaa vya Reli Wizi vifaa vya Reli

Jeshi la Polisi Kikosi cha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne katika maeneo ya Temeke Veternari jijini Dsm wakidaiwa kuhujumu miundombinu ya Reli hiyo yenye thamani ya Shilingi Milioni 6.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Tazara, SACP, Mwamini Marco, amesema watu hao wamekamatwa baada ya kufanyika kwa msako katika reli ya TAZARA kuanzia Dsm hadi Mkoa wa Songwe na kuwabaini wakiwa na vipande 80 vya reli.

Amesema Jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vitaendelea na operesheni ya kuwasaka wahalifu watakaojihusisha na uhujumu wa reli huku wakiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa lengo la kuboresha ulinzi na usalama ndani ya reli hiyo.