Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 04Article 541009

Habari za Mikoani of Friday, 4 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Yanga SC upepo mbaya wavuma

Yanga SC upepo mbaya wavuma Yanga SC upepo mbaya wavuma

Bumbuli amenukuliwa akisema Yanga ikajiandaa na mechi nne tu za Ligi Kuu Tanzania Bara ambazo ni dhidi ya Ruvu Shooting itakayochezwa Juni 17, Mwadui FC (Juni 20),  Ihefu (Julai 14) na Dodoma Jiji itakayofanyika  Julai 18 ambayo ni siku ya funga pazia.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa aliliambia gazeti hili jana klabu yao inaheshimu makubaliano yaliyofikiwa katika kikao cha mwisho walichokutana wakiwamo viongozi wa Serikali, TFF na Bodi ya Ligi.

Mfikirwa alisema kauli hiyo iliyotolewa na Bumbuli haikuwa rasmi na kusisitiza Yanga inaheshimu ratiba ambayo imetolewa na itaifuata.

“Viongozi hatujatoa tamko lolote kuhusu mchezo wetu dhidi ya Simba, tunaheshimu ratiba iliyopangwa na Bodi ya Ligi  na TFF, aliyoyasema Ofisa Habari wetu yasipewe kipaumbele kwa sababu ameongea kama ilivyo kwa mashabiki na makomandoo wengine," alisema Mfikirwa.

Kiongozi huyo alisema bado wanaendelea na vikao vya ndani kwa ajili ya kuweka mipango ya mechi zao zilizobakia ikiwamo mchezo huo wa watani wa jadi na mtanange wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA ambao watakutana na Biashara United.

Aliwataka mashabiki wao kuendelea kusubiri tamko rasmi la klabu ambayo imedhamiria kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika michezo yote iliyopo mbele yao.

"Jumatatu (wiki hii), wachezaji wote waliingia kuendelea na maandalizi ya mechi zetu hizo, kasoro nyota wawili ambao ni Sogne Yacouba na Mukoko Tonombe ambao wameondoka kwenda kujiunga na timu zao za Taifa,” alisema Mfikirwa.

Aliongeza benchi la ufundi limependekeza kupata mechi tatu za kirafiki na Jumapili wataanza kucheza dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini.

Join our Newsletter