Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 28Article 544549

Diasporian News of Monday, 28 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Yasin Rais mpya ZFF

Yasin Rais mpya ZFF Yasin Rais mpya ZFF

MKUTANO Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar, ZFF, limemchagua Abdul-latif Ali Yasin kuwa Rais wao.

Yasin alishinda katika uchaguzi huo kwa kupata kura 16 Kati ya kura 24 zilizopigwa kwenye uchaguzi huo, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo Kilimani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Katika uchaguzi huo, wagombea watano waliwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Rais wa Shirikisho hilo, Seif Kombo Pandu kujiuzulu, ambapo matokeo ya awali yalishindwa kupata mshindi kutokana na kutokufikia asilimia kwa mujibu wa Katiba.

Katika matokeo ya awali, Abdul Latif Yasin alipata kura 11, akifuatiwa

na Suleiman Shaaban ambae alipata kura saba na Suleimana Mahmoud Jabir alipata kura sita na wagombea wawili Abdulkadir Mohammed Abdulkadir ‘Tashi’ na Haji Shehe hawakupata kura hata moja, matokeo ambayo yaliufanya uchaguzi huo kurejewa.

Katika marudio ambao wagombea walibakia wawili kati ya

Abdul-latif Ali Yasin na Suleiman Shaaban, yakamchaguwa Yasin kuwa Rais kwa kupata kura 16 kati ya kura 24 sawa na asilimia 67 na Suleiman kura nane sawa na asilimia 33.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia

Uchaguzi huo, Fadhil Ramadhan Mberwa alisema uchaguzi huo uliwashirikisha wapiga kura 24 na kumchaguwa Rais huyo, ambaye atatumikia nafasi hiyo kumalizia kipindi kilichobaki cha miaka miwili.

Mapema kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo kulifanyika Mkutano Mkuu

ambao ulifunguliwa na Kaimu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Lela Mohamed.