Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 14Article 557323

Habari Kuu of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb/WHO

Zaidi ya watu 700,000 wanajiua kila mwaka, Tanzania iko nafasi ya 27 Afrika

Zaidi ya watu 700,000 wanajiua kila mwaka, Tanzania iko nafasi ya 27 Afrika Zaidi ya watu 700,000 wanajiua kila mwaka, Tanzania iko nafasi ya 27 Afrika

Imeelezwa kuwa kila mwaka, takribani watu 700,000 hufariki kwa kujiua na bado idadi ya watu wanaojaribu kujiua ikiongezeka siku hadi siku duniani kote.

Taarifa ya Shirika la Afya Duniani, WHO, imeeleza kuwa kujiua ni chanzo namba nne cha idadi ya cifo vyote vinavyotokea duniani kote kila siku na wanaothirika zaidi ya maamuzi haya ni vijana wadogo wenye umri wa miaka 15 hadi 19.

Nchini Tanzania tatizo la watu kujiua pia limechukua sura mpya siku za karibuni ambapo kwa mujibu wa World Health Ranking Tanzania imetajwa kushika nafasi ya 82 duniani kwa idadi ya vifo vya kujiua na 27 kwa Afrika.

Vifo vya kujiua vimekua vikiathiri zaidi familia, jamii na nchi zenye idadi kubwa ya watu wanaochukua maamuzi hayo kila wakati na kupelekea kubaki na nyakati ngumu na zisizosahaulika kwa waliobaki.

Kujiua hakutokei tu kwenye nchi zenye uchumi mkubwa, janga hili limezikumba nchi zote duniani na kwa mujibu wa taarifa za WHO, dunia nzima imekumbwa na vifo vya watu kujia kwa asilimia zaidi ya 77 hadi kufikia mwaka 2019.

Kujiua limeshakua tatizo kubwa kwenye jamii, hata hivyo kujiua kunazuilika endapo tatizo litawahiwa kwa hatua mbalimbali kuchukulia ikiwemo serikali na jamii kuweka mikakati ya kusaidia wananchi kupambana na msongo wa mawazo.