Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 21Article 558775

Habari za Afya of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Zaidi ya watu milioni 80 Afrika wamepokea chanjo COVID-19

Zaidi ya watu milioni 80 Afrika wamepokea chanjo UVIKO-19 Zaidi ya watu milioni 80 Afrika wamepokea chanjo UVIKO-19

Ripoti iliyotolewa na Hospitali ya John Hopkins ya mjini New York nchini Marekani, tarehe 21,Septemba ,2021 imeonesha idadi ya maambukizi ya Ugonjwa wa UVIKO-19 kufika milioni 81.16, huku idadi ya waliopokea chanjo imetajwa kuwa milioni 80.59 katika bara la Afrika.

Ripoti hiyo pia imeonesha idadi ya vifo vilivyo tokana na ugonjwa huo barani humu kufika laki 206,332, huku idadi ya waliopona ni milioni 7.46.

Hata hivyo imeitaja nchi ya Afrika Kusini kushika chati katika kasi ya maambukizo ya UVIKO-19 ambapo visa takribani milioni 2.88 vimeripotiwa huku kukiwa na vifo vipatavyo elfu 86,216.

Mataifa mengine yanayo ongoza kwa idadi ya visa vya ugonjwa huo, ni Morroco ikiwa na visa 920,374, Tunisia 700,400, Libya 332026, Ethiopia 333,698 , Misri wao wakiwa na matukio 297,608 pamoja na Kenya yenye visa 246,643.