Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 24Article 573883

Habari Kuu of Wednesday, 24 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Zanzibar yasaini mikataba uendeshaji uwanja wa ndege kimataifa

Zanzibar yasaini mikataba uendeshaji uwanja wa ndege  kimataifa Zanzibar yasaini mikataba uendeshaji uwanja wa ndege kimataifa

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetia saini mikataba minne na kampuni nne za kimataifa ya uendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa Amani Abeid Karume.

Hafla ya utiaji mikataba hiyo imefanyika leo Jumatano Novemba 24, 2021 ikishuhudiwa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi Ikulu visiwani humo.

Mikataba hiyo imesainiwa baina ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) na kampuni za kimataifa za Dnata, Eg's Emirates na Segap, inahusu kutoa huduma za abiria na mizigo, uendeshaji wa uwanja wa ndege, kumbi na maduka na migahawa vilivyomo ndani ya uwanja huo.

Akizungumza kabla ya kutia saini mikataba hiyo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Zanzibar, Rahma Kassim Ali amesema lengo ni kuimarisha huduma za uwanja huo wenye uwezo wa kuhudumia watu milioni 1.5 Kwa mwaka.

"Wizara imeona kuna haja ya kushirikiana na wataalamu hawa ambao wanauzoefu mkubwa katika masuala haya ili kuboresha zaidi huduma za uwanja wetu," amesema Waziri Rahma

Amesema, kwa muda mrefu wamekuwa na changamoto viwanja vya Ndege hivyo kusababisha hata kudorora kwa uchumi.

"Tunaahidi wizara itatoa mashirikiano katika shughuli zote za uendeshaji wa uwanja huu lengo ni kuleta tija na kuongeza watalii wanaokuja hapa nchini,"