Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 08Article 556228

Siasa of Wednesday, 8 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Zitto kabwe akutana na Katibu Mkuu CCM

Mwenyekiti wa TCD, Zitto Kabwe, akiwa na Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo Mwenyekiti wa TCD, Zitto Kabwe, akiwa na Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo

katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Daniel Chongolo amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Zitto Kabwe.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 08 Septemba, 2021 Makao Makuu ya CCM Dodoma, ambapo Zitto aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Lawrence Malawa.

Pamoja na mambo mengine, Mazungumzo hayo yamelenga zaidi kujitambulisha kwa Mwenyekiti mpya wa TCD Ndg. Zitto Kabwe alieyechaguliwa mwezi Agosti mwaka huu.

Zitto alikabidhiwa majukumu hayo kutoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa kituo hicho, James Mbatia, Agosti 26 mwaka huu, na tayari amesha vitembelea vituo vya haki za binadamu pamoja na Asasi za kiraia kwa ajili ya kujitambulisha.