Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573493

Habari Kuu of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

kila baada ya sekunde 24 mtu mmoja hufariki kwa ajali ya gari- UN

kila baada ya sekunde 24 mtu mmoja hufariki kwa ajali ya gari kila baada ya sekunde 24 mtu mmoja hufariki kwa ajali ya gari

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kila sekunde ishirini na nne mtu mmoja anakufa kwenye ajali ya barabarani duniani.

Amesema hayo katika Maadhimisho ya Siku ya Kukumbuka Waliopoteza Maisha au kujeruhiwa kutokana na ajali za barabarani.

Amesema katika kuadhimisha siku hiyo ni wakati wa kutafakari juu ya vifo vilivyosababishwa na ajali za barabarani.

Ameitaka kila nchi, kampuni na raia duniani isaidie juhudi za kitaifa na kimataifa za kuhakikisha barabara zinakuwa salama zaidi hususani kwenye nchi za kipato cha chini na kati ambako zaidi ya asilimia tisini ya vifo vinavyotokana na ajali barabarani hutokea.