Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 28Article 560149

Soccer News of Tuesday, 28 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

28/09/2021: Ratiba mechi zote za leo, Ligi Kuu Bara

Ratiba michezo ya Ligi, Septemba 28 Ratiba michezo ya Ligi, Septemba 28

Ligi Kuu Bara inaendelea kuchanja mbuga baada ya jana Septemba 27 kuanza kasi kwa timu tatu kupambana kusaka pointi tatu.

Leo Septemba 28, Ligi hiyo itaendelea kwa kushuhudia mechi tatu katika Viwanja viatatu tofauti.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes itakuwa Uwanja wa Karume, Mara bila uwepo wa nyota wao kadhaa akiwemo Taddeo Lwanga ambaye alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa, Septemba 25.

Mbali na mchezo huo unaosubiriwa kwa shauku kubwa pia Dodoma Jiji itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Pia kuna mchezo mwingine ambapo Mbeya City itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine.