Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 09Article 584443

African Cup of Nations of Sunday, 9 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

AFCON 2021 Kuanza Leo Cameroon

Michuano ya AFCON itafunguliwa pazia leo Januari 9 Michuano ya AFCON itafunguliwa pazia leo Januari 9

Maandalizi yamekamilika kuelekea michuano ya soka kwa mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Cameroon, iliyoahirishwa kutoka mwaka 2021 kwa sababu ya janga la Covid 19.

Nyota kadhaa wa Ligi Kuu na Ulaya watashuka dimbani Cameroon, huku wenyeji wakimenyana na Burkina Faso katika mchezo wa ufunguzi.

Kwa mara ya kwanza michuano hiyo ilihairishwa kuchezwa Juni 2021 na kusogezwa mbele hadi Januari mwaka jana ili kuepusha msimu wa mvua nchini Cameroon, michuano hiyo imecheleweshwa hadi 2022 kwa sababu ya janga la corona.

Kombe la Mataifa Africa AFCON itakuwa na washiriki 24 kwa amara ya pili mfululizo ikiwa na makundi sita ya timu nne, huku mbili za juu zikifuzu kwa hatua ya 16 bora sambamba na timu nne zilizo kwenye nafasi ya tatu bora.

Michezo ya AFCON itafanyika majira ya saa 16:00, 19:00 na 22:00 (muda wa EAT) wakati wa awamu ya makundi, na nyakati mbili zitatumika katika awamu ya mtoano kuanzia Jumapili, 23 Januari.