Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 12Article 585085

Soccer News of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

#AFCON: Sarkodie Ataka Kuvunja TV Yake Morocco Ikiipiga Ghana

#AFCON: Sarkodie Ataka Kuvunja TV Yake Morocco Ikiipiga Ghana #AFCON: Sarkodie Ataka Kuvunja TV Yake Morocco Ikiipiga Ghana

VIDEO iliyozua hisia imesambaa mitandaoni ikionyesha rapa maarufu raia wa Ghana Michael Owusu Addo, almaarufu Sarkodie akikosa utulivu akitazama mechi ya Timu ya Taifa ya Ghana 'Black Stars' dhidi ya Morocco 'Atlas Lions of Morocco' katika michuano ya Kombe la AFCON.

Rapa huyo anaonyeshwa akichachawa huku Black Stars wakizidiwa na mabingwa hao wa Kaskazini mwa Afrika.

Ghana ilipoteza mechi hiyo na kichapo cha 1-0 katika Kundi C na michuano hiyo, na kumvunja moyo mshindi huyo wa BET alikosa utulivu akitazama mechi hiyo.

Miamba hao wa Magharibi mwa Afrika walichezea kichapo kutoka kwa Morocco, baada ya bao la dakika ya lala salama kutoka kwa Sofiane Boufal na kuizamisha jahazi la Waghana.

Katika video iliyopakiwa kwenye Twitter na SportsBrief.com, Sarkodie anaonekana akiweweseka baada ya bao hilo huku akitaka kuvunja runinga yake aliyokuwa akitazama mchezo huo.

Sarkodie alikuwa na matumaini makubwa kabla ya mechi hiyo kuwa Ghana itashinda;
"Penda usipende hisia hii ninayopata wakati nchi yangu inacheza," aliandika kwenye Twitter.

Black Stars wanasaka taji la tano la Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kushinda mara ya mwisho mnamo mwaka 1982.