Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 11Article 585067

African Cup of Nations of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

#AFCONCAMEROON: Algeria yalazimishwa sare na Sierra Leone

Algeria vs Sierra Leone zaenda sare ya bila kufungana Algeria vs Sierra Leone zaenda sare ya bila kufungana

Mabingwa watetezi wa Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021 wameanza taratibu katika mashindano hayo baada ya kutoa sare tasa na Sierra Leone mchezo uliopigwa Leo ukiwa wa kwanza katika Kundi E.

Wasumbufu Sierra Leone walikuwa kwenye ubora mkubwa ungwe ya kwanza ambapo mshambuliaji wa Leone Alhaji Kamara alipata nafasi ambazo alikuwa kwenye uwezo wa kuipatia uongozi timu yake.

Hata hivyo, Algeria kama Mabingwa watetezi walionyesha ubora kipindi cha pili ambapo fowadi Yacine Brahimi alijaribu kwa shuti kali lakini kipa Mohamed Nbalie Kamara alibaki imara.

Ikiwa ni mara ya kwanza kucheza mechi za AFCON kwa Sierra Leone tangia mwaka 1996, walicheza pamoja na kwa umoja ambapo sasa wanafanikiwa kumaliza mechi bila kuruhusu goli licha ya kukwaruzana na timu bora.