Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 19Article 552487

Soccer News of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: Mwanaspoti

AS Vita kuwaandaa Wanigeria wa Yanga

Rivers United Rivers United

Rivers United ya Nigeria inayoanza na Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, itashiriki michuano mifupi nchini Benin ambayo AS Vita ya DR Congo ni moja ya washiriki.

Rivers United wamethibitisha kushiriki michuano hiyo ya Chalenji ya Afrika Magharibi, na wataitumia kuipima timu kujiandaa na msimu mpya.

Michuano hiyo imepangwa kuanza leo Alhamisi mpaka Jumatano ijayo nchini Benin, huku timu shiriki ni Hearts of Oak (Ghana),Union Sportive de la Gendarmerie Nationale (Niger), Horoya Athletic Club (Guinea), Arta Solar 7 (Djibouti), Loto-Popo FC (Benin), Vita Club (Congo) na AS Sonabel FC (Burkina Faso). Zipo nyingine ni Les Buffles (Benin) na Rivers United FC (Nigeria).