Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 11Article 584833

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Aaron Ramsey akutwa na Uviko-19

Aaron Ramsey Aaron Ramsey

klabu ya juventus imekumbwa na wingu zito baada ya habari mbaya kuibuka baada ya kiungo wao Aaron Ramsey kukutwa na maambukizi ya Uviko-19 na atahitajika kujitenga kwa siku 14.

Aaron Ramsey hajaonekana kwenye kikosi tokea huu mwaka 2022 uanze, hivi karibuni kocha Max Allegri alitoa kauli ya kumfungulia njia ya kutokea kwenye dirisha hili la usajili, “yuko njiani kuondoka kwenye hii klabu”.

Aaron Ramsey ambaye kwa sasa amejitenga kutokana na matibabu ya Uviko-19, wiki iliyopita klabu ya Juve ilikumbwa na maambukizi ya wachezaji watatu wenye Uviko-19 ambao ni Chiellini, Arthur and Pinsoglio, ila kwa sasa wote wamepona,

Ramsey alisajiriwa kama mchezaji huru akitokea klabu ya nchini Uingereza Arsenal mwaka 2019 majira ya kiangazi, tokea asajiriwe hajaweza kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye klabu hiyo.

Sasa Aaron Ramsey anahusishwa na vilabu vya Newcastle United na Aston Villa vyote vya uingereza, pia Ramsey na Juve mkataba wao unafika tamati mwaka 2023.