Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 26Article 574111

Soccer News of Friday, 26 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Aggrey Moris Ageukia Ukocha

Aggrey Moria ageukia ukocha Aggrey Moria ageukia ukocha

Nahodha wa klabu ya Azam FC Aggrey Morris ni Miongoni mwa washiriki wa Kozi ya Ukocha ya CAF Diploma C ambayo inaendelea Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Karume, Ilala, Dar es Salaam.

Ikumbukwe kuwa, Aggrey ni miongoni mwa wchezaji waandamizi wa Azam ambao wamepewa adhabu ya kusimamishwa kuitumikia klabu hiyo kwa muda usiojulikana kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu. Wenzake waliosimamishwa ni Sure Boy na Mudathiri Yahya.

Aggrey pia amestaafu kwa heshima kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars hivi karibuni.

Nini maoni yako, unadhani ni wakati sahihi sasa kwa Aggrey kustaafu kucheza soka na kujikita kwenye ukocha zaidi?