Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573295

Soccer News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Aguero kustaafu soka kwa changamoto ya moyo

Sergio Kun Aguero Sergio Kun Aguero

Hali ya mshambuliaji wa FC Barcelona, Sergio Aguero sio njema sana kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya moyo. na hivyo anafikiria kuachana na mchezo wa mpira wa miguu.

Aguero amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo kwa muda sasa na hivi karibuni, alipata shida hiyo akiwa uwanjani tukio lililopelekea mchezaji huyo kuwaishwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Taarifa zimeripoti kuwa, Sergio Aguero anauwezekano wa kustaafu soka kutokana na afya yake kwa sasa. Maamuzi haya yameshafanyika na Barcelona wameshapatiwa taarifa ya tukio hilo kutokea.

Wiki ijayo kuna uwezekano wa kufanyika mkutano na wanahabari kuhusu kustaafu kwa Aguero na hapo, taarifa kamili itatolewa na pande zote zinazohusika.

Aguero amekuwa nje tangu alipotolewa dakika za mapema kwenye mchezo waliotoa suluhu ya goli 1-1 na Alaves Oktoba 30.