Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573127

Habari za michezo of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Ajenda 11 kujadiliwa mkutano wa Simba

Ajenda 11 kujadiliwa mkutano wa Simba Ajenda 11 kujadiliwa mkutano wa Simba

Hali ya utulivu imetawala wakati mchakato wa kuhakiki kadi za wanachama kwenye mkutano mkuu wa Simba ikiendea asubuhi hii kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.

Ajenda 11 zitajadiliwa kwenye mkutano huo ikiwamo ya mapendekezo ya marekebisho ya kanuni za uchaguzi na katiba za klabu ya Simba.

Mkutano huo uliochelewa kwa takribani saa moja ulitarajiwa kuanza majira ya saa 3:00 za asubuhi, huku wanachama wakiendelea kumiminika kushiriki mkutano huo.

Hadi kufikia saa 3:40 eneo la ukumbi wa chini ulikuwa umejaa huku watu wa itifaki wakitakiwa kuwaongoza wanachama wanaoendelea kuwasili ukumbini hapa kwenye viti vya eneo la juu la ukumbi huo.