Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 13Article 585466

African Cup of Nations of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Algeria Watoa Kisingizio cha Kubanwa na Sierra Leone

Algeria Watoa Kisingizio cha Kubanwa na Sierra Leone Algeria Watoa Kisingizio cha Kubanwa na Sierra Leone

Wachezaji wa timu ya taifa ya Algeria wamesema sababu kubwa ya kufanya vibaya na kubanwa mbavu na Sierra Leone katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021 ni hali kali ya joto nchini Cameroon ambayo wanadai kuwa iliwaathiri.

Algeria kama Mabingwa watetezi wa Kombe hilo walikuwa wanatumainiwa kushinda mechi hiyo lakini haikuwa hivyo kwani timu ya Cape Verde iliyo kwenye viwango vya Fifa vya 108 ilionyesha ubabe na kuibana vilivyo.

“Ilikuwa hali ngumu sana kwetu, hasa sisi ambao tunaocheza Ulaya. Hatujazoea hali ya joto kama hii,” alisema kiungo Haris Belkebla.

“Tumeumia sana”.

Beki wa kushoto Ramy Bensebaini, naye pia alisema “hali ilikuwa haieleweki mana joto kali” kauli ambayo imeungwa moto na Steven Caulker beki wa Leone ambaye pia aliunga mkono hoja ya hali ya joto Cameroon ilikuwa shida.

Mechi ijayo kwa Algeria itakuwa dhidi ya Equatorial Guinea Jumapili ambapo timu ya taifa hiyo inatajwa kuwa kipaumbele cha kutwaa ubingwa.