Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 14Article 551479

Soccer News of Saturday, 14 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Ambokile arejeshwa Mbeya City, Haule bado kidogo tu

Straika Mpya wa Mbeya City, Eliud Ambokile Straika Mpya wa Mbeya City, Eliud Ambokile

Mbeya. Wakati joto la usajili likizidi kupamba moto kwa timu mbalimbali hapa nchini, Mbeya City inatajwa kumalizana na nyota wanne, huku ikiwa hatua za mwisho kumnasa Kipa wa Azam, Benedict Haule kwa mkopo.

Timu hiyo ya jijini hapa katika msimu uliopita licha ya kumaliza nafasi ya 10, lakini haikuwa na mwanzo mzuri hadi kusubiri mechi mbili za mwisho na kujihakikishia kukusanya alama 42.

Taarifa ilizopata Mwanaspoti kutoka ndani ya klabu hiyo ni kuwa tayari imekamilisha usajili wa nyota wapya wanne akiwamo aliyekuwa Straika na mfungaji wake wa muda wote, Eliud Ambokile.

Wengine waliosaini hadi sasa ni Straika wake wa zamani, Paul Nonga kutoka Gwambina, Pato Ngonyani (Polisi Tanzania) na Frank Ikibela aliyerejeshwa tena kikosini kutoka Ruvu Shooting.

Hata hivyo inadaiwa kuwa timu hiyo inatarajia kutangaza usajili wake kuanzia wiki ijayo pamoja maandalizi ya jumla ya msimu ujao ikiwamo kambi ambayo inatazamiwa kuanza Agosti 26 mwaka huu.