Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572467

Mpira wa Kikapu of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Antentokounmpo awaadhibu LA Lakers

Giannis Antentokoumpo (kushoto) Giannis Antentokoumpo (kushoto)

Burudani ya mchezo wa kikapu inaendelea viwanjani. Msimu wa 2021/22 kunako NBA ni visa na mikasa. Vipigo vya kila namna kwa wasiotegemewa kupoteza michezo.

Milwaukee Bucks walikuwa uwanjani kuchuana na LA Lakers alfajiri ya leo. Lakers hali ni mbaya msimu huu, wanapoteza michezo mfululizo kwa mara ya 3 msimu huu.

Giannis Antentokoumpo amekuwa mwiba msimu huu. Nyota huyu raia wa Ugiriki, alipachika jumla ya pointi 47 kati ya 109 zilizowapa ushindi Bucks. Lakers wameendelea kumkosa LeBron James ambaye ana majeraha msimu huu.

Pamoja na kumkosa James, Lakers walipachika pointi 102 zilizochangiwa kwa sehemu kubwa na Talen Horton-Tucker (pointi 25) na Russell Westbrook (pointi 19).

Kwingineko kwenye NBA; Brooklyn Nets wameshinda kwa pointi 109-99 dhidi ya Cleverland Cavaliers. Phoenix Suns wamewafunga Dallas Mavericks kwa pointi 105-98. Charlotte Hornets wameibuka kidedea kwa vikapu 97-87 dhidi ya Washington Wizards.