Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 20Article 572983

Soccer News of Saturday, 20 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Antonio Conte kama wengine tu kwa Ndombele

Ndombele bado hajawapa uhakika wa matokeo bora Tottenham Ndombele bado hajawapa uhakika wa matokeo bora Tottenham

Linapotajwa jina Tanguy Ndombele, ujue ni mchezaji ghali kuwahi kusajiliwa Tottenham Hotspurs. Antonio Conte ni kama makocha waliomtangulia kwenye hili.

Ndombele amekuwa akizua gumzo kwa nafasi yake ndani ya uwanja. Mauricio Pochettino, Jose Mourinho na Nuno Espirito Santo, wote wamepata tabu na mchezaji huyu. Uwezo wake ni mkubwa sawa, lakini nini anakifanya uwanjani hilo ni suala jingine.

Antonio Conte hana muda mrefu toka ametua Spurs lakini, hajasita kutoa neno kwa Ndombele. Hii ni dhahiri, Conte ameshawajua baadhi ya wachezaji wake na pengine kikosi kamili cha kocha huyu, kitadhihirika siku si nyingi.

Kuelekea mchezo dhidi ya Leeds United, Conte amesema haya kwa Ndombele;

"Nimewaona makocha wengi wakipata shida na nafasi yake. Anaubora lakini, anapaswa kuelewa hii ni timu na anatakiwa kuitumikia timu".

"Kila mchezaji anatakiwa kujua nini anachotakiwa kukifanya. Kama kila mchezaji atakua anakimbia tu uwanjani, hizo ni vurugu" amesema Conte