Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 01Article 554854

Soccer News of Wednesday, 1 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Antonio Nugaz Atemwa Yanga SC

Aliekua Afisa muhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Antonio Nugaz Aliekua Afisa muhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Antonio Nugaz

Aliekuwa Afisa muhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Jumaa Khatibu Nugaz maarufu kama "Antonio Nugaz" ameachana na Klabu hiyo yenye maskani yake Jangwani baada ya kumaliza Mkataba wake wa Miaka miwili.

Taarifa hiyo imetolewa na klabu ya Yanga kupitia mitandao yake ya kijamii leo Septemba 1, 2021.

Kwa upande wake Nugaz pia ameushukuru Uongozi wa Yanga katika kipindi chote alichofanya nao kazi.

Tukio hilo la Nugaz limekuja siku chache tangu Klabu hiyo ipate Msemaji mpya alietokea Klabu ya Simba SC, Haji Sunday Manara.

Aidha siku tatu ama nne zilizopita, Nugaz katika mtandao wake wa Instagram alipost "video clip" inayomuonesha akifurahi na mashabiki wa Yanga huku akimuita jina ambalo sio Sahihi msemaji mpya wa Yanga, tukio ambalo linasemekana kuwakera Viongozi wa juu wa Klabu ya Yanga.

Sehemu ya taarifa ya klabu ya Yanga SC.