Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 27Article 559801

Soccer News of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Arsenal mtaielewa tu, yaichapa Tottenham goli 3

Aubameyang akishangilia goli dhidi ya Tottenham Aubameyang akishangilia goli dhidi ya Tottenham

Washika bunduki wa London, Arsenal ni kama wameshakaa kwenye mstari baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya wakali wengine kutoka London Totenham Hotspurs.

Katika mchezo huo Arsenal walionyesha kiwango bora na kuibuka na ushindi mnono hatimaye wakashusha presha kwa kocha Mikel Arteta ambae alikuwa na mwanzo mbaya wa msimu.

Magoli ya Arsenal katika mchezo huo yamefungwa na Smith- Rowe, Aubameyang na Bukayo Saka na yote yamefungwa kipindi cha kwanza.

Goli pekee la Tottenham limefungwa na Son dakika za mwishoni mwa mchezo na mapaka dakika 90 zinakamilika Arsenal wakaibuka na ushindi katika mchezo huo wa London Derby.