Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 14Article 551482

Soccer News of Saturday, 14 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Arsenal ndio kama mlivyosikia

Wachezaji wa Brentford wakishangilia moja ya magoli yao Wachezaji wa Brentford wakishangilia moja ya magoli yao

Mafahari wa Jiji la London,klabu ya Arsenal imejikuta ikianza vibaya ufunguzi wa pazia la Ligi kuu ya England, baada ya kukubali kichapo cha bao 2-0 kutoka kwa wageni wa Ligi hiyo.

Klabu ya Brentford ambao wamepanda daraja, imewaadhibu wababe hao katika mechi ya kwanza bila kujali ugeni wao katika ligi hiyo yenye ushindani wa hali ya juu.

Vijana wa Thomas Frank, wakiwa kwenye Uwanja wao wa Nyumbani, Brentford Community, hawakupewa nafasi ya kunyakua pointi tatu kutokana na ugeni wao lakini mpaka dakika 90 zinakabilika Vijana wa Mikel Arteta walikua hoi huku ubao ukisoma 2-0, na magoli ya Brebford yalifungwa na Sergi Canos (22') na norgaard (73').

Klabu ya Arsenal kwa miaka ya hivi karibuni haijafanyi vizuri na hasa tangu kuondoka kwa kocha wake wa muda mrefu Arsene Wenger, wana miaka zaidi ya kumi hawajabeba taji la Epl huku wengi wakiona kama watashindwa kupata matokeo basi mkufunzi wao Mikel Arteta ataonyeshwa mlango wa kutokea.