Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 12Article 585304

Soccer News of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Aston Villa yawalaza chali Chelsea

Lucas Digne Lucas Digne

Aston Villa wanajambo lao kwenye dirisha la usajili Januari hii. Hakika, Steven Gerard anapata msaada mkubwa kutoka kwa viongozi wa klabu hiyo. Chelsea wamelala chali!

Villa wapo mbioni kukamilisha usajili wa Lucas Digne akitokea Everton. Ni dhahiri, uhusiano wa Digne na kocha wa Everton, Rafael Benitez ulishavunjika. Kwa sababu hizi, Digne aliamua kumueleza wazi Benitez kuwa anataka kuondoka klabuni hapo mwezi huu.

Miongoni mwa timu zilizokuwa zikimuwinda Digne ni Chelsea na West Ham United. Everton waliweka wazi, Digne hatotolewa kwa mkataba wa mkopo, yeyote anayemtaka amsajili kwa mkataba wa moja kwa moja.

The Blues na The Hammers, wote wameshindwa kufua dafu kwa Aston Villa. Lucas Digne huenda akatangazwa leo kama usajili wa pili baada ya Philippe Countinho. Villa na Everton wameafikiana kuhusu usajili wa Lucas Digne ambapo, dau la £25M limeafikiwa na pande zote mbili.

Ni suala la muda tu kabla Lucas Digne hajaonekana kwenye uzi wa Villa na, kunauwezekano akawavaa Manchester United wikiendi hii.