Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 08Article 561994

Soccer News of Friday, 8 October 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Aucho amtibulia ulaji Okwi

Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho

Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho amezidi kung’aa na sasa baada ya kutamba nchini amehamishia ufalme hadi kwao Uganda akimtibulia staa wa zamani wa Simba.

Akiwa katika kiwango bora tangu atue Yanga, Aucho amemtibulia mshambuliaji wa zamani wa Simba Emmanuel Okwi akichukua cheo chake katika timu ya taifa lao la Uganda ‘The Cranes’.

Kocha wa Uganda, Sredojevic Milutin ‘Micho’ amempa Aucho kitambaa cha unahodha wa timu hiyo katika kikosi kilichoshuka uwanjani jana kucheza dhidi ya Rwanda.

Micho baada ya kumWita Okwi katika mechi mbili dhidi ya Mali na Kenya akiwa kama nahodha tangu astaafu kwa kipa Denis Onyango safari hii amemuacha katika kikosi cha sasa ambapo.

Sababu kubwa ya kuachwa kwa Okwi, Mwanaspoti linafahamu mshambuliaji huyo amekuwa hana timu kwa sasa tangu kuachana na El Ittihad ya Misri baada ya mkataba wake kumalizika.

Hata hivyo, juzi usiku Okwi alitua Rwanda akikaribia kujiunga na klabu ya Kiyovu ya nchini humo akiwa kama mchezaji huru.

Endapo Okwi atamalizana na Kiyovu dili hilo linaweza kufuta uwezekano wa mshambuliaji huyo kurejea Simba ambao walikuwa wanampigia hesabu.