Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 19Article 558250

Soccer News of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Azam FC, Biashara United zapeperusha vyema bendera ya Tanzania

Wawakilishi wa Tanzania Kombe la Shirikisho, Azam na Biashara United Wawakilishi wa Tanzania Kombe la Shirikisho, Azam na Biashara United

Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Timu za Azam FC na Biashara United zimefanikiwa kushinda michezo yake ya mikondo ya pili ya hatua za awali za Kombe la Shirikisho Afrika.

Azam FC ndio waliokuwa wa kwanza kushuka dimbani katika dimba la Azam Complex Chamazi Jijini Dar es Salaam, majira ya saa 10 jioni kuvaana na timu ya Horseed FC kutoka kule nchini Somalia.

Katika mchezo huo ambao Azam walikua wageni, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Ismail Aziz 38', na hivyo kufanya Azam kuibuka na ushindi wa jumla wa magoli 4-1 (mchezo wa awali walishinda 3-1).

Katika mchezo mwingine majira ya saa 1:00 usiku, Wanajeshi wa Mpakani, Biashara United nao wamefanikiwa kusonga mbele baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Dikhil FC kutoka nchini Djibout, (mchezo wa awali Biashara alishinda 1-0). Magoli ya Biashara United yamewekwa kimiani na Mkongwe Ramdhan Chombo 19' na 23', na kwa matokeo hayo timu zote mbili Azam na Biashara zimefanikiwa kusonga mbele katika hatua inayofuata(hatua ya kwanza) ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Azam FC watakutana na Pyramids FC ya nchini Misri, mwezi Oktoba wakati Biashara United watakutana na mshindi kati ya Al wadi vs Al Ahli Tripoli.