Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 21Article 558742

Habari za michezo of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Azam FC Waipotezea Pyramids

Azam FC. Azam FC.

BAADA ya kufuzu hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika kocha wa Azam FC, George Lwandamina amesema kuwa kwa sasa akili yao wanaelekeza kwenye Ligi Kuu Bara.

Lwandamina amesema hawawezi kuwaza mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa sababu upo mbele zaidi tofauti na michezo ya ligi kuu.

Azam walifanikiwa kusonga mbele baada ya kupata ushindi wa jumla wa mabao 4-1 mbele ya Horseed FC ya Somalia wakishinda 3-1 kwenye mchezo wa kwanza na kisha 1-0 kwenye mechi ya pili.

Mchezo ujao Azam watakumbana na wababe wa Misri, FC Pyramids timu ambayo iliwahi kuiondosha Yanga.

Lwandamina alisema: “Nafikiri kwa sasa tunatakiwa kuwaza zaidi mechi za ligi kuu, kwa sababu ndiyo sehemu tunayokwenda, ikifika wakati wa mechi za kimataifa tutafanya hivyo pia.”