Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 13Article 551398

Soccer News of Friday, 13 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Azam FC haoo Zambia

Wachezaji wa Kikosi cha Azam FC Wachezaji wa Kikosi cha Azam FC

Baada ya Simba na Yanga kutangaza kuweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao nchini Morocco, wababe wenzao Azam wamewakwepa na kupanga kupiga kambi nchini Zambia katika jiji la Ndola.

Taarifa zinasema kuwa awali Azam walikuwa na mapendekezo mawili ya kambi ambapo walipanga kwenda nchi moja kati ya Afrika Kusini na Zambia na kuyachakata na hatimaye huenda siku za hivi karibuni wakasafiri kwenda Zambia sehemu ambayo aliipendekeza kocha mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina.

Maandalizi hayo yamepangwa kuanza wiki ijayo kama mambo yataenda vizuri na timu tayari ipo kambini Chamazi, ikijifua tangu Jumatatu ya wiki hii ikisubiri taratibu za kwenda Zambia zikamilike.

Kwana namna inavyyoneka Azakma wamefunga hesabu kwenye usajili wa wachezaji wa kimataifa na sasa wako kwenye harakati za kunasa nyota wasiozidi watatu wa ndani kisha kwenda Zambia.

“Usajili wa wachezaji wa kigeni tumemaliza, tumebakiza nafasi chache tu za wachezaji wa ndani ambao kwa sasa siwezi kuwataja,” alisema.