Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 25Article 553507

Soccer News of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Azam FC kazi kazi

Wachezaji wa Azam FC wakifanya mazoezi Zambia Wachezaji wa Azam FC wakifanya mazoezi Zambia

Kikosi cha Azam FC kimeenda Zambia kujifua kwa ajili ya Msimu mpya wa ligi na kombe la Shirikisho Afrika.

Kikosi cha Matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam kitakaa kwa siku 12 na kitacheza michezo minne na watachjeza kila baada ya siku mbili kabla ya kurejea nchini kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Mapema Septemba.

Kikosi hicho kinajifua mara mbili kwa siku kuhakikisha wanakua fiti kwa mapambano ya msimu mpya wa ligi. Na wanapiga mzigo asubuhi na jioni.

Miongoni mwa mechi watakazocheza Azam za kujipima nguvu ni dhidi ya Zesco United na Zanaco zote za nchini Zambia.