Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 25Article 553648

Soccer News of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Azam FC kushuka dinbani leo

Wachezaji wa Azam FC wakifanya mazoezi Zambia Wachezaji wa Azam FC wakifanya mazoezi Zambia

Klabu ya Azam FC itacheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki nchini Zambia leo majira ya Saa 10:00 Jioni kwa saa za hapa nyumbani Tanzinia. Watacheza dhidi ya Red Arrows ukiwa ni mchezo wao wa kwanza kati ya michezo minne ya kirafiki watakayoicheza wakiwa huko Zambia.

Kikosi hicho cha matajiri wa jiji la Dar es salaam kiliondoka nchini Jumatatu ya Agosti 23, 2021, kuelekea Ndola Zambia ambako kimeweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano (Pre-season) kuelekea msimu wa 2021-22.

Kikosi hicho kikiwa huko kitacheza michezo minne ya kirafiki na mchezo wa kwanza ni wa leo dhidi ya Red Arrows, ambayo ni timu ya jeshi la anga la Zambia.

Agosti 29 wataminyana na Zanaco, timu ya benki ya Taifa ya biashara, Septemba 2 watacheza mchezo wa tatu dhidi ya Forest Rangers, timu ya mamlaka ya uhifadhi misitu. Na Septemba 3 watacheza mchezo wa mwisho dhidi ya Zesco, ambayo ni timu ya shirika la Taifa la umeme nchini Zambia.   Na Septemba 5, 2021 kikosi hicho kitarejea nchini kwa maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho barani Afraka dhidi ya Horseed FC ya Somalia.