Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 30Article 560539

Soccer News of Thursday, 30 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Azam FC mikononi mwa maafande, Ubingwa unawezekana?

Azam FC, watakutana na Polisi Tanzania Oktoba 2 Azam FC, watakutana na Polisi Tanzania Oktoba 2

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati, ameweka wazi kuwa malengo makubwa ya timu yao msimu huu wa 2021/22 ni kuhakikisha wanashinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara kama ilivyokuwa msimu wa 2013/14

Azam FC mchezo wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu mpya wa 2021/22 ilianza kwa kugawana pointi moja moja na Coast ugenini.

Baada ya dakika 90, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ubao ulisoma Coastal Union 1-1 Azam FC hivyo wameacha pointi mbili sawa na wenyeji wao.

Bahati amesema “Baada ya kuwa na mwanzo mzuri katika Kombe la Shirikisho Afrika ambapo timu yetu imefanikiwa kufuzu hatua ya kwanza, sasa ni muda wa kurejea kwenye mashindano mengine muhimu ambayo ni Ligi Kuu Bara.

“Tumekuwa na maandalizi mazuri ya kabla ya msimu, pia tumefanya usajili bora kwa msimu huu wa 2021/22, malengo yetu makubwa ni kushinda ubingwa wa Ligi Kuu, kwa ubora wa kikosi chetu tunaamini hilo linawezekana.”

Mchezo wao ujao kwenye Ligi Kuu Bara ni dhidi ya Polisi Tanzania ambayo ilianza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC kwenye mchezo uliochezwa jana, Septemba 29, Uwanja wa Karatu.

Azam FC inaarajiwa kumenyana na Polisi Tanzania, Jumamosi ya Oktoba 2. Tayari kikosi kimeweka kambi Moshi na kinaendelea na maandalizi kuelekea kwenye mchezo wao wa mzunguko wa pili.