Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 30Article 554410

Soccer News of Monday, 30 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Azam FC ngoma imetiki

Wachezaji wa Azam wakimpongeza Dube baada ya kufunga goli dhidi ya Kabwe Warriors Wachezaji wa Azam wakimpongeza Dube baada ya kufunga goli dhidi ya Kabwe Warriors

Kikosi cha Matajiri wa Jiji Azam FC ambao wako kule Ndola, nchini Zambia wakiwa wameweka kambi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara na Kombe la Shirikisho Afrika.

Kikosi hicho kimecheza mchezo wake wa pili wa kirafiki na kuondoka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Straika wao hatari Prince Dube kipindi cha pili dakika ya 59'.

Huenda ndio tayari mipango ya Mwalimu Lwandamina imeshaanza kuingia tayari kwani katika mchezo huo Azam wameonekana kuelewana kwa kiasi kikubwa huku wakitengeneza nafasi za kutosha.

Kikosi cha Azam FC kimeweka Kambi yake ya kujiandaa na msimu ndola nchini Zambia na kambi hiyo itawachukua siku 12, huku wakijiandaa kucheza michezo minne ambapo tayari wamekwishacheza miwili na iliyobaki ni dhidi ya Vigogo wa Soka nchini humo Zesco United na Zanaco FC.