Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 12Article 556972

Soccer News of Sunday, 12 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Azam FC ngoma imetiki, yawachapa wasomali goli 3

Wachezaji wa Azam wakimpongeza Idris Mbombo Wachezaji wa Azam wakimpongeza Idris Mbombo

Matajiri wa Jiji Azam FC, wameibuka na ushindi mnono wa goli 3-1 katika mchezo wao wa awali wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya timu ya Horseed FC kutoka Somalia. Azam FC ambao ndio waliokuwa wenyeji wa mchezo huo, wamecheza mechi bila ya Mashabiki baada ya Shirikisho la Soka Afrika CAF, kupiga marufuku mahudhurio ya Mashabiki viwanjani ikiwa ni katika harakati za kupambana na Janga la Virusi vya Corona.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex magoli ya wenyeji yamefungwa na Ayoub Lyanga 32', Idrisa Mbombo 73' na Lusajo Mwaikenda 78', huku lile la Horseed FC likifungwa na Ibrahim Nor 22'.

Mechi ya Mkondo wa pili baina ya Timu hizo itapigwa Septemba 18, katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, ambapo Azam FC watakua wageni.

Hatua hiyo ya Horseed FC kutumia Uwanja wa Uhuru kama uwanja wa Nyumbani imekuja baada ya hali ya Usalama nchini Somalia kutokua ya kuridhisha.