Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 26Article 553876

Soccer News of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Azam FC wakumbana na Kipigo Zambia

Mchezaji wa Azam akijaribu kumtoka Mchezaji wa Red Arrows Mchezaji wa Azam akijaribu kumtoka Mchezaji wa Red Arrows

Matajiri wa Jiji Azam FC, ambao wako kule Ndola nchini Zambia walipoweka kambi ya takriban siku 12 kujiandaa na msimu wa 2021/2022, wamekumbana na kipigo kitakatifu katika mechi yao ya kwanza kujipima ubora wa kikosi chao.

Katika mechi hiyo dhidi ya Red Arrows, Azam FC walipoteza kwa goli 4-0 huku wakitawaliwa kwa kiasi kikubwa na wapinzani wao.

Katika mechi hiyo ambayo ilichezwa kwa vipindi vitatu vya dakika 30, Azam wamekubali kuona mapungufu yao na watafanyia kazi ili kufanya vyema katika mechi inayokuja.

akizungumza kwa njia ya simu kutokea Zambia, Afisa habari wa Azam, Thabiti Zakaria amesema;

"Hawa wenzetu wameanza mazoezi muda mrefu hivyo tayari wameshakaa sawa, Mwalimu amesema sisi ndio kwanza tuko katika mazoezi ya kujenga mwili kwa hiyo tunakwenda taratibu na tutakaa sawa".

Azam itacheza mechi nne za kujipima huku Zesco United na Zanaco zikiwa ni miongoni mwa timu watakazocheza nazo.