Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 20Article 552778

Soccer News of Friday, 20 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Azam FC wapo tayari kwa Mashindano

Wachezaji wa Azam FC wakijifua mazoezini Wachezaji wa Azam FC wakijifua mazoezini

Kikosi Matajiri wa Jiji, Azam FC kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kwa msimu wa 2021/22 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ameweka wazi kwamba kila kitu kipo sawa na wanahitaji kufanya vizuri.

"Tupo tayari kwa ajili ya msimu mpya na tuna amini kwamba tutafanya vizuri hivyo mashabiki watupe sapoti,".

Msimu uliopita wa 2020/21 Azam FC ilimaliza ikiwa nafasi ya tatu na pointi 68.

Pia kwa ajili ya msimu ujao leo wamezindua uzi wao mpya ambao watautumia katika mechi ambazo watashiriki kwenye Ligi Kuu Bara.