Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 29Article 560380

Soccer News of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Azam FC watua Kilimanjaro, waisoma Polisi Tanzania

Sehemu ya Kikosi cha Azam FC Sehemu ya Kikosi cha Azam FC

Mabosi wa Jiji la Dar es Salaam, Azam FC kwa sasa wapo ndani ya ardhi ya Kilimanjaro kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Polisi Tanzania.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumamosi,Oktoba 2,2021 ikiwa ni kwa ajili ya msimu wa 2021/22.

Azam FC wanaingia kwenye mchezo wa pili wakiwa na kumbukumbu ya kugawana pointi mbele ya Coastal Union kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja Mkwakwani.