Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 10Article 584773

Soccer News of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Azam haoo Fainali Mapinduzi Cup, Yanga chali

Mudathir Yahaya akipongezwa baada ya kufunga penati ya ushindi Mudathir Yahaya akipongezwa baada ya kufunga penati ya ushindi

Matajiri wa Jiji Azam FC,wamefanikiwa kutinga hatua ya Fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup 2022 wakimuondosha bingwa mtetezi Yanga.

Dakika 90 zilimalizika kwa sare ya bila kufungana na hivyo mchezo huo uliamuliwa kwa njia ya matuta.

Azam wametinga hatua ya Fainali kwa ushindi wa penati 9-8 dhidi ya Yanga, huku beki wa kushoto Yasin Mustapha akikosa kwa upande wa Yanga.

Azam wanamsubiri mshindi kati ya Simba na Namungo wanaocheza mishale ya saa mbili usiku.