Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 08Article 584320

Soccer News of Saturday, 8 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Azam yaifuata Yanga Kibabe Nusu Fainali Mapinduzi Cup

Azam FC itakutana na Yanga nusu Fainali siku ya Jumatatu Azam FC itakutana na Yanga nusu Fainali siku ya Jumatatu

Timu ya Azam FC imekamilisha mechi zake za Kundi A Kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya wenyeji, Yosso Boys jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo mawili dakika ya 40 kwa penalti na 66, beki Mghana Daniel Amoah dakika ya 51, kiungo mzawa, Ismail Aziz Kada dakika ya 57 na Munzil Abdallah aliyejifunga dakika ya 74, wakati bao pekee la Yosso Boys limefungwa na Daudi Francis Hiluka dakika ya 19.

Kwa ushindi huo, Azam FC inamaliza na pointi tisa kileleni mwa Kundi A, na sasa itamenyana na washindi wa Kundi B na mabingwa watetezi, Yanga katika Nusu Fainali, wakati washindi wa pili wa Kundi A, Namungo FC watacheza na washindi wa Kundi C, Simba SC mechi zote zitachezwa Jumatatu na Fainali itafuatia Alhamisi.