Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 28Article 544576

Habari za michezo of Monday, 28 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Azam yakiri uzembe kufungwa bao Simba

Azam yakiri uzembe kufungwa bao Simba Azam yakiri uzembe kufungwa bao Simba

Katika mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Majimaji mjini Songea, Simba ilibidi kusubiri hadi dakika ya 88, kupata bao hilo pekee la kuongoza baada ya Bernard Morrison kuchezewa madhambi nje kidogo ya 18 na kuipiga faulo haraka kwa Miquissone ambaye aliuzamisha mpira kimyani wakati wacheazaji wa Azam FC wakimfuata mwamuzi kupiga adhabu hiyo.

Baada ya bao hilo, wachezaji wa walizonga refa wakipiga bao hilo lakini Morris, akizungumzia mchezo na na bao hilo alisema: Ni kweli mechi ilikuwa ngumu kwa pande zote mbili ila dakika za mwisho tulizembea, wenzetu wameanza mpira haraka, tumefungwa."

Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati: “Niwapongeze Simba wamepata ushindi dakika za mwisho, ingawa nina mashaka na goli, mpigaji kama alipiga ndani ya boksi, na faulo ilichezwa nje ya boksi."