Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 27Article 559993

Soccer News of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Azam yalazimishwa sare Mkwakwani, Mtibwa hoi

Wachezaji wa Azam wakisaka Goli dhidi ya Coastal Union, Mkwakwani Tanga Wachezaji wa Azam wakisaka Goli dhidi ya Coastal Union, Mkwakwani Tanga

Matajiri wa Jiji, Timu ya Azam FC wamelazimishwa sare katika mechi yao ya kwanza ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/2022.

Katika mchezo huo Azam ndio wliokuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza kupitia kwa Danie Amoah dakika ya 49 ya mchezo baada ya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana.

Huku ikiwa kama imeshaonekana mechi imemalizika Wagosi wa kaya Coastal Union wakapachika goli la kusawazisha dakika ya 90 kupitia kwa Hance Masoud na kuwaacha Azam wasiamini wanachokiona.

Mpaka Dakika 90 zinakamilika mechi hiyo imeisha kwa sare ya bao 1-1.

Matokeo mengine katika Ligi hiyo katika mchezo wa mapema kule katika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, wageni wa Ligi kuu timu ya Mbeya Kwanza imeitandika Klabu ya Mtibwa Sugar goli 1-0 na kuwafanya waanze vyema harakati za kugombea ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara.

Goli pekee la Mbeya Kwanza limewekwa wavuni na Willy Edgar dakika ya 49.