Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 26Article 544396

Habari za michezo of Saturday, 26 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Baba Samatta afunguka kuhusu mtaa aliopewa mwanaye

Baba Samatta afunguka kuhusu mtaa aliopewa mwanaye Baba Samatta afunguka kuhusu mtaa aliopewa mwanaye

UKITAKA kuamini soka linalipa muulize supastaa, Mtanzania Mbwana Samatta, anayekipiga kwa mkopo Fenerbahçe namna anavyorejeshewa heshima na jamii, baada ya kuwapa burudani safi.

Samatta yupo nchini, hivi karibuni alikwenda kuzindua mtaa uliopo Kibiti ambao umepewa jina lake 'Samatta Street', jambo ambalo alilishukuru kuona Watanzania wameamua kutunza vya kwao.

Katika mtandao wake wa kijamii (instagram), aliandika "Mcheza kwao hutunzwa, asante sana Watanzania kwa kunipa heshima kubwa ya mtaa wenu kuupa jina langu,". mwisho wa kunukuu.

Mwanaspoti Online limezungumza na baba mzazi wa mwanasoka huyo, Ally Pazi Samatta amesema walikwenda kuuzindua mtaa huyo jana Ijumaa na tukio hilo lilihudhuriwa na viongozi wa mtaa huo.

"Kiukweli nimejisikia faraja kubwa kama mzazi kuona kijana wangu anaona heshima ya Watanzania akiwa hai, inampa nguvu ya kupambana zaidi akiamini Watanzania wanampenda;

Ameongeza kuwa "Mbwana ana tabia ya ukimya, akashukuru sana lakini kama mzazi namjua nilipoitazama sura yake nikaiona ile furaha yake inayotoka ndani, nipende kuwashukuru Wanakibiti kwa moyo wao wa upendo, pia kuna mtaa ambao alipewa Kigoma,"amesema.