Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 20Article 552733

Soccer News of Friday, 20 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Balama apewa Program Maalum Morocco

Mchezaji wa Yanga, Mapinduzi Balama Mchezaji wa Yanga, Mapinduzi Balama

Licha ya kuwepo kambini nchini Morocco, lakini kiungo mshambuliaji wa Yanga, Balama Mapinduzi, ataendelea kufanya mazoezi binafsi kwa ajili ya kujiweka fiti.

Kiungo huyo yupo nje ya uwanja kwa muda wa mwaka mzima akiuguza majeraha ya mfupa wa kifundo cha mguu aliyoyapata msimu wa 2019/2020.

Akizungumza na Spot Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, amesema Balama atakuwepo sehemu ya kikosi hicho kwa msimu ujao baada ya kupona majeraha yake hayo.

Mwakalebela amesema kuwa, kiungo huyo hivi sasa yupo katika program maalum ya mazoezi kambini huko Morocco chini ya uangalizi wa madaktari wa timu hiyo.

“Balama amepona majeraha yake ya enka yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu, hiyo ndiyo sababu ya kumjumuisha katika msafara wetu wa Morocco ambako tumeweka kambi".

“Atakuwa sehemu ya kikosi chetu tutakachokitumia msimu ujao baada ya kupona na ili acheze anatakiwa kupona kwa asilimia mia moja, hivyo ataendelea na program hiyo kwa kipindi chote tutakachokuwepo hapa kambini Morocco huku akisubiri majibu ya madaktari,” amesema Mwakalebela.